Kuhusu Sisi

DIRA YETU

Kuhakikisha Zanzibar inakuwa nchi inayoongoza kwenye maendeleo ya michezo kwa nchi za Afrika ya Mashariki na kati.


DHAMIRA YETU

Kuratibu na kusimamia maendeleo ya michezo kwa ajili ya kuleta Umoja, Amani, Utulivu, Ajira na Maendeleo endelevu ya kuibua na kuendeleza vipaji ili vishiriki katika mashindano na kuleta heshima kwa Zanzibar.

KAZI ZETU

Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na kanuni za Michezo.
Kuandaa na kusimamia mpango mkuu wa maendeleo ya Michezo Zanzibar.
Kuwa kiungo kati ya Serikali na wadau wengine wa michezo ndani na nje ya nchi.
Kujenga na kuendeleza miundombinu ya michezo.
Kusimamia haki, maslahi, afya na maendeleo ya wachezaji na viongozi wa michezo.
Kusimamia na kuendeleza timu za Taifa.

Motos