Ifahamu Idara ya Michezo

Idara ya Michezo ilianzishwa mwaka 2002 baada ya kutenganishwa na iliyokua Kamisheni ya Utamaduni na Michezo ikiwa dhamira kuu ni kusimamia ipasavyo shughuli za kimichezo Zanzibar na hatimaye kuiwezesha Zanzibar kuwa nchi inayoongoza kwenye Maendeleo ya michezo kwa Nchi za Afrika ya Mashariki na kati .

Mara baada ya kuanzishwa kwa Idara hiyo, Raisi wa Awamu ya Saba Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alimteuwa Nd.Sharifa Khamis Salim kuwa Kamishna wa Idara hiyo hadi 2020.

Kwa Sasa Idara ya Michezo inaongozwa na Nd.Ameir Mohamed Makame amabaye aliteuliwa kuwa Kamishna wa Idara hiyo Tarehe 24/05/2021.

Idara ya Michezo ni miongoni mwa Idara muhimu sana kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na majukumu yake iliyopangiwa ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu ya michezo na kusimamia mpango mkuu wa maendeleo ya Michezo ili kutimiza malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuimarisha Michezo kama ilivotajwa katika ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na kufikia malengo ya kuwainua vijana katika suala la kimichezo .

Idara ya Michezo ipo chini ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Muheshimiwa Tabia Maulid Mwita ambapo idara hii makao makuu yake yapo ndani ya Kiwanja cha Mao Zedong Kikwajuni Zanzibar.

Viwanja Vyetu

Kwa sasa Zanzibar ina viwanja vitatu vya kitaifa ambavyo ni Amaan, Mao Zedong na Gombani Pemba.

Uwanja wa Amaani.

Uwanja huu Umefunguliwa na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius K.Nyerere Tarehe 12/01/1970 .

Soma Zaidi

Uwannja wa Mao Zedong

Uwnja huu ulifunguliwa rasmin tarehe 03/01/2019 na Rais wa awamu ya Saba Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

Orodha ya Oda